Mwanamuziki wa Hip Hop Bongo, Stamina ametumia siku ya wanawake duniani kwenda kwa mama wa mtoto wake kwa kusema ni mpambanaji sana katika maisha yake.

Stamina amesema kuwa mwanamke wake huyo ni mpambanaji pia alikuwa anakaa getini kukusanya pesa wakati anafanya show mikoani.

Stamina amesema alishangazwa na kitendo hicho kwani hakutegemea kama mpenzi wake huyo atafanya jambo hilo kwa zaidi ya mikoa 15.

Amesema kuwa “Ukiachana na mama mzazi siku ya wanawake duniani naipeleka kwa Mama Lionel, kipindi nakutana naye sikutegemea kama ni mpambanaji.

 Stamina amesema kuwa mwanamke huyo alimshangaza kwani nilikuwa na ziara zangu za chaka kwa chaka za mikoani akasema twende wote, yeye alikuwa anakaa getini kuchua pesa wakati nafanya show kwenye jukwaa na alikuwa anawakazia kinoma noma.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *