Muigizaji wa Nollywood, Ramsey Nouah amefunguka na kueleza kuwa anamkumbuka msanii wa Bongo movie marehemu Steven Kanumba kwa sababu ndiye aliyejenga daraja la ushirikiano kati yao.

Kanumba alijaribu sana kuipeleka bongo movie kimataifa zaidi kwa kutafuta wasanii mbali mbali wa nje ya nchi na kushirikiana nao iki kukuza sanaa kwa kipindi hiko.

Ramsey amekiri kuwa Kanumba ndiye aliyewezesha ushirikiano kati ya Nollywood na Bongo movie. Yeye na Kanumba walicheza movie mbili pamoja ambazo ni Devils Kingdom na Moses.

Ramsey amekuja nchini Tanzania kwa ajili ya kushiriki kwenye kongamano la kutambua fursa kwa vijana nchini kwa mualiko wa Sahara Tanzania.

Lakini Ramsey hakuishia hapo alisisitiza kuwa siku ya Jumamosi ataenda kutembelea kaburi la Marehemu Kanumba na kuwasihi Watanzania wote waungane naye.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *