Aliyekuwa Mwenyekiti wa Wanawake CCM (UWT), Sophia Simba amerejeshewa uanachama wa CCM baada ya kuomba radhi.
Sophia Simba alifukuzwa uanachama wa CCM kwenye kikao cha kamati kuu ya chama kilichofanyika mapema mwaka huu mkoani Dodoma.
Mwenyekiti wa CCM Rais John Magufuli amesoma barua ya Sophia kuomba radhi mbele ya Kikao cha Halmashauri Kuu ya CCM (NEC) na kuwahoji wajumbe kama wanakubali kumsamehe jambo lililokubaliwa.
Rais Magufuli amesema kuwa Sophia Simba aliandika barua ya kuomba radhi mara nyingi lakini walikuwa wakikaa kimya ila kwasasa wameamua kuisoma mbele kikao hicho na wanachama kukubali arejeshwe.
Baada ya kuwahoji wajumbe na kukubaliwa Rais Magufuli aliandika kwenye barua hiyo kuwa amekubaliwa kurudi CCM.