Mwanamuziki wa Singeli nchini, Snura amesema kuwa ameshangaza sana kuona wimbo wake ‘Nimevurugwa’ kufungiwa na Mamlaka ya Mawasiliano nchini ‘TCRA’ wakati ni wimbo wa muda mrefu.
Snura amesema kuwa ameshangazwa sana na kitendo hiko wakati wimbo huo ameuachia muda mrefu sana ukilinginisha na nyimbo zake nyingine kama vile chura ambao nao pia umefungiwa kwa kukosa maadili katika jamii.
Kauli hiyo ya Snura imekuja kufuatia Mamlaka ya Mawaliano nchini kuzifungia nyimbo 13 baada ya kupokea orodha ya nyimbo za wasanii zilizokosa maadili kutoka Baraza la Sanaa Tanzania (BASATA).
Snura anasema kuwa wimbo wa nimevurugwa ni wa zamani sana ukilinganisha na nyimbo yake ya chura na hata za wengine zilizofungiwa kwa sababu ni za hivi karibuni.
Kufungiwa kwa nyimbo hizo ni muendelezo wa kazi ya BASATA likiwa na nia ya kufungia na kukataza nyimbo zote na wasanii wote ambao wamekuwa wakitoa nyimbo au kuchapisha picha ambazo hazina maadili.