Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Snura Mushi ameishtaki kampuni moja ya usambazaji wa unga nchini baada ya kampuni hiyo kutumia wimbo wake wa Majanga katika tangazo lao la biashara bila idhini yoyote kutoka kwake.

Snura anasema kuwa kampuni iyo inayoshughulika na bidhaa za unga imetumia wimbo wake wa majnaga katika matangazo yao lakini yeye hakuwa na taarifa zozote kama mmiliki hiyo inabidi kampuni iyo imlipe fidia kwa kosa ilo.

Amesema kuwa tayari alishatafuta mwanasheria na mwanasheria huyo alishawatumia ‘notice’ kampuni hiyo ya unga kuwa ndani ya siku saba wawe tayari wameshamlipa fidia yake inayokadiriwa kuwa ni bilioni 2.1 kwa kutumia wimbo huo.

Pia Snura amesema kuwa kesi hiyo imesota kwa muda wa zaidi ya mwaka sasa na ameshaangaika sana na kutafuta wanasheria mara tatu zaidi, na alitumia baadhi ya mamalka husika na bado hakuweza kufanikiwa kwa chochote.

Snura hatokuwa msanii wa kwanza kupeleka kampuni mahakamani, hivi karibuni kulikuwa na kesi nyingine mahakani iliyohusisha kampui ya tigo na wasanii Ay na Mwana Ka kutokana na kutumia nyimbo zao kwa miito ya simu kwa wateja bila kuwa na ridhaa yao.

Makampuni yamekuwa vikitumia nyimbo za wasanii katika shuguli zao bila kuwa na hati miliki kutoka kwa msanii husika.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *