Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Snura Mushi amesema kwa sasa kila anapoandika wimbo au kutoka kutoa ni lazima awasiliana na Baraza la Sanaa Taifa (Basata).

Snura amesema kuwa analazimika kufanya hivyo ili kuepuka hasara anayopata pindi nyimbo zake zinapofungiwa na Basata kama nyimbo yake ya chura ilivyofungiwa kutokana na kukosa maadili katika jamii.

Pia amesema kuwa muda mwingi hadi akirekodi huwa anapiga simu sababu ya kufanya hivyo hataki tena nyimbo zake kufungiwa.

Wimbo wa Snura ‘Chura’ ulifungiwa na Baraza la Sanaa nchini (BASATA) kutoka na kwenda kinyume na maadili katika jamii.

Mwanamuziki huyo kwasasa anatamba na wimbo wake mpya unaokwenda kwa jina la ‘Vumbi la Mguu’ unaofanya vizuri katika vituo vya radio na tv nchini.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *