Mwanamuziki wa Marekani, Snoop Dogg ameweka wazi kwamba hajawahi kupiga Kura kumchagua kiongozi katika maisha yake yote.

Snoop amesema hakuwahi kufata haki yake hiyo ya Kikatiba kutokana kupumbazwa kwamba hawezi kufanya hivyo kwa sababu ya rekodi zake za makosa ya jinai.

Amesema kuwa “Sijawahi kupiga Kura kwenye maisha yangu, lakini mwaka huu nitapiga Kura kwa sababu siwezi kuvumilia kumuona yule mpuuzi Rais Trump pale ofisini.

Kwa miaka mingi walikuwa wakinipumbaza nakufikiri kwamba ‘huwezi kupiga Kura kutokana na rekodi za makosa ya jinai’ Sikufahamu. Sasa naweza kupiga Kura” alisema Snoop Dogg.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *