Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) iko mbioni kuanzisha mfuko wa hija  kuwawezesha Waislamu wasiokuwa na uwezo lakini wana nia ya kwenda kutekeleza ibada ya hija.

Katika hotuba  yake  ya  Baraza  la  Iddi jana, Rais  wa  Zanzibar  na  Mwenyekiti  wa  baraza la  Mapindunzi, Dk. Ali  Mohamed Shein  alisema  mfuko  huo  pia utasaidia  wastaafu  ambao wamekuwa  wakitumia  fedha  zao  za  kiinua  mgongo kwa  ajili  ya  kwenda  kutekeleza ibada  ya  hija     Makka,  Saudia Arabia.

Dk. Shein  aliyaeleza  hayo  katika  ukumbi  wa  Chuo  cha  Mafunzo  ya Amali Mkanyageni  Wilaya  ya  Mkoani,  Mkoa  wa  Kusini  Pemba  alipozungumza  na waumini  wa  dini ya kiislamu waliohudhuria   baraza  la  Iddi  ambalo  kitaifa limefanyika  kisiwani humo.

Ili kufanikisha suala hilo, Dk. Shein  alizitaka  taasisi  zinazojihusisha na kupeleka  mahujaji  kushirikiana  na  Serekali kupitia  Kitengo  cha  Wakfu  na  mali  amana   kuhakikisha waislamu wanaokwenda kufanya ibada ya hijja  wanakwenda  na  kurudi  salama.

Alisema     Sh  bilioni 16 .2  zimelipwa     kwa wastaafu 1,193 na kati  yao,  90 wamepewa  fursa  maalum  kwa  ajili ya kwenda  kutekeleza ibada  ya  hija  ambayo  ni  nguzo  mojawapo  katika nguzo  za  kiislamu.

Dk. Shein pia aliwaasa Waislamu kuendelea kudumisha amani ya nchi kwa kutii sheria ambayo ndiyo msingi katika kuleta mshikamano wa wananchi hivyo kufikia maendeleo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *