Aliyekuwa mpenzi wa Nay wa Mitego, Siwema Edson amefunguka kuwa kama asingepitia misukosuko ya kimapenzi na mzazi mwenziye huyo mpaka kuachana basi asingepata akili ya kujibidiisha kibiashara.

Siwema amesema baada ya kupata misukosuko alitafakari na kuamua kupiga moyo konde na kusimama kama mwanamke ili afanye kitu ambacho kitamsimamisha na kuendelea na maisha yake.

“Unajua ukikumbwa na misukosuko hasa ya kimapenzi akili inatanuka, nilijiongeza haraka na leo hii nina duka langu kubwa la nguo hapa Mwanza na maisha yanaendelea, ningekaa kulilia mapenzi ningechemka,”.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *