Mkuu wa Jeshi la polisi nchini, IGP Simon Sirro amesema kuwa jeshi hilo halina lengo la kuwakamata wanasiasa kwa kuwaonea ila linawakamata watuhumiwa kutokana na makosa yao.
Sirro amesema kuwaΒ endapo ushahidi utaonyesha hawahusiki na jambo walilokamatiwa wataachiwa huru kwa mujibu wa kanuni na sheria za nchi.
IGP Sirro ameyasema hayo mkoani Tanga alipozungumza na waandishi wa habari baada ya kumaliza mkutano wake alioufanya na askari wa jeshi hilo mkoani humo.
Kamanda Sirro ametoa kauli hiyo baada ya wapinzani kulalamika kuwa jeshi la Polisi linawaonea sana viongozi wa upinzani kwa kuwakamata wakati wa utekelezaji wa kazi zao.
Sirro yupo mkoani Tanga kwa ziara maalum mkoani humo ambapo alikagua gwalide la jeshi la Polisi akiwa mkoani hapo.