Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), George Simbachawene amesema kuwa sababu zilisababisha mikoa saba kushindwa kutimiza utengenezaji wa madawati ni kucheleweshwa kwa uteuzi wa viongozi katika mikoa hiyo.

Simbachawene amesema amegundua tatizo kubwa lililosababisha kucheleweshwa kwa zoezi hilo ni kucheleweshwa kwa uteuzi katika nafasi mbalimbali, pamoja na mawasiliano mabovu katika safu za uongozi wa mikoa.

madawati

Waziri huyo mwezi Novemba mwaka jana ametoa muda hadi Januari 2017 mikoa hiyo iliyokuwa na upungu iwe imekamilisha zoezi hilo na kusema kuchelewa kwa uteuzi wa makatibu tawala na wakurugenzi kumechangia kwa kiasi kikubwa mipango mingi kutofanyika kwa wakati ikiwemo hiyo ya madawati.

Mikoa iliyokuwa imepewa muda huo, na wakuu wake kuelezwa kuwa ni pamoja na mkoa wa Geita, Mwanza, Kigoma, Mara, Dodoma, Rukwa na Simiyu.

Pia amekiri uwepo wa upungufu wa vyumba vya madarasa ambapo amesema kuwa baada ya zoezi la madawati kukamilika, sasa nguvu zinahamia kwenye vyumba vya madarasa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *