Klabu ya Simba ya jijini Dar es Salaam imeingia mkataba wa miaka mitano na kampuni ya michezo ya kubashiri ya SportPesa ambao una thamani ya Sh. bilioni 4.9.

Mkataba huo, utaifanya Simba ipokee kitita cha Sh milioni 888 katika mwaka wa kwanza baada ya kuingia mkataba huo.

Mmoja wa Wakurugenzi wa SportPesa, Abbas Tarimba amesema Simba itapewa Sh bilioni 1 na milioni 80 katika mwaka wa mwisho wa mkataba kwa kuwa kila mwaka, fedha 5% zitakuwa zinaongezeka katika mkataba.

Pia Simba imeambiwa kama itachukua ubingwa basi ina nafasi ya kuchukua Sh milioni 100 kama zawadi au pongezi kutoka SportPesa.

Kampuni hiyo pia  imetenga Sh milioni 250 wakibeba Kombe la Kagame au michuano iliyo chini ya Caf.

Udhamini huo unakuwa ndiyo mkubwa zaidi kuliko mingine yoyote ambayo Simba imewahi kuingia ikidhaminiwa.

Mkataba huo unaifanya Simba kuwa timu isiyo na hasara kama ilivyo kwa msimu huu ambao imemaliza ikicheza bila ya kuwa na mdhamini mkuu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *