Ligi kuu Tanzania Bara imeendelea leo katika viwanja tofauti hapa nchini ambapo Simba SC imefanikiwa kuifunga Azam FC 1-0 kwenye mechi iliyofanyika katika uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.
Goli pekee la Simba limefunga na Shiza Kichuya katika dakika 67 ya mchezo na kuisadia Simba SC kupata alama tatu muhimu na kufikisha alama 13 katika michezo mitano iliyocheza mpaka sasa.
Katika hatua nyingine Yanga SC imeifunga Mwadui 2-0 kwenye mechi iliyofanyika katika uwanja wa Kambarage mkoni Shinyanga na kuifanya timu hiyo kufikisha alama 10 katika michezo minne iliyocheza.
Magoli ya Yanga yamefungwa na Amissi Tambwe kipindi cha kwanza na Donald Ngoma kipindi cha pili.
Matokeo ya mechi nyingine za Ligi Kuu leo, Mbao FC imepata ushindi wa kwanza baada ya kuifumua Ruvu Shooting 4-1 Uwanja wa Mabatini, Mlandizi, Pwani, Ndanda FC wameshinda 2-1 dhidi ya wenyeji Maji Maji Uwanja wa Maji Maji, Songea na Mtibwa Sugar wameshinda 2-0 dhidi ya Kagera Sugar wakati Mbeya City imetoka sare ya 0-0 na Prisons Uwanja wa Sokoine, Mbeya.
Ligi Kuu inatarajiwa kuendelea kesho kwa mchezo kati ya Stand United na JKT Ruvu Uwanja wa Kambarage mkoani Shinyanga wakati Jumanne African Lyon wataikaribisha Toto Africans ya Mwanza.