Yanga na Simba wanatarajia kumenyana katika mechi ya kwanza kesho Jumamosi Oktoba mosi kwenye mechi ya ligi kuu Tanzania bara itakayofanyika katika uwanja wa taifa jijini Dar es salaam.
Timu hizo zimejikita kambini kujiandaa kwa mechi hiyo ,Simba mpaka sasa ndio wanaongoza ligi baada ya kucheza Mechi 6 na wana pointi 16 wakifuatiwa na Stand United wenye Pointi 12 kwa Mechi 6.
Nafasi ya tatu ni inashikiliwa na Yanga huku nafasi za nne na tano zipo Azam FC na Mtibwa Sugar zote zikiwa na pointi 10 kila mmoja.
Katika kuelekea mechi hiyo makocha wa timu hizo Joseph Omong wa simba na Hans van Pluijim, kila mmoja amesema kuwa timu itaibuka na ushindi.
Msimu uliopita, Yanga iliifunga Simba mabao 2-0 katika mechi zote mbili zilizofanyika katika uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.