Waziri wa Mambo ya Ndani, Mwigulu Nchemba ameshiriki zoezi la kuteketeza silaha haramu 5,608 zilizokamatwa kwenye matukio ya kihalifu na zingine kusalimishwa hapa nchini.

Waziri Nchemba ameandika katika ukurasa wake wa Instagram, “Tanzania hatuungi mkono wa umiliki wa silaha haramu.Hapa tukiteketeza silaha haramu.”

haramu2

Nchema amewaomba wananchi kuendelea kuliunga mkono jeshi la polisi. “Tuendelee kutoa ushirikiano kwa jeshi letu kufichua watu wanaomiliki silaha isivyo kihalali”.

Silaha hizo haramu zimeteketezwa na jeshi la polisi mkoani Kigoma ambapo silaha nyingi zilihusika katika uhalifu nchini pamoja na nyingine zimesalimishwa na baadhi ya waharifu hao baada ya kubainika.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *