Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Harmonize amewaomba radhi mashabiki wake nchini Kenya kutokana na kushindwa kufanya shoo baada ya promota kuingia mitini.
Shoo hiyo ilitakiwa kufanyika jana El Derot nchini Kenya na kushindwa kufanyika hivyo ikamlazimu Harmonize kuomba radhi mashabiki zake wa nchi hiyo.
Sakata hilo lilitokea baada ya Harmonize kushindwa kupanda jukwaani kutumbuiza baada ya Promota aliyemleta kushindwa kumalizia mkwanja wake kama walivyopatana.
Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Harmonize ameandika ujumbe wa kuwaomba radhi mashabiki ambao walitoa pesa nyingi kununua tiketi lakini wamejikuta wakikosa shoo kutoka kwa Harmonize.
Harmonize anakuwa msanii wa pili kuwanyooshea vidole mapromota feki kutoka nchini Kenya kwani miezi michache iliyopita tu msanii kutoka Nigeria Tiwa Savage alilalamikia suala hilo.