Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Shilole ametangaza kugombe ubunge kwenye jimbo la Igunga mkoani Tabora kwenye uchaguzi mkuu utakafanyika mwaka huu.
Kwa mujibu wa Shilole ameandika kuwa amekuwa muwakilishi mzuri wa Igunga hivyo endapo akipewa Jimbo hilo basi ataliongoza vyema kutokana uhodari wake.
Kupitia ukurasa wake wa Instagram ameandika ‘Mimi Shishi ambaye ni mbunge kivuli wa mda mrefu wa kujitolea wa jimbo langu la Igunga na ambaye sipo rasmi bungeni kwasasa.
Naisubiria kwa hamu kubwa siku isiyokuwa na tarehe lakini ni mwezi wa kumi jumapili moja hivi asubuhi ya mwaka huu 2020 baada ya ibada ya kwanza, ni siku ambayo nitatangazwa rasmi kama mbunge mwakilishi wa jimbo la Igunga.
Nimefanikiwa kuiweka Igunga kwenye ramani nzuri ya Tanzania bila ya kuwa mbunge rasmi kwahiyo sitashindwa kuifanyia maendeleo Igunga yangu nikiwa mbunge rasmi pale mjengoni. Wazee na Vijana kwa pamoja nipokeeni kijana wenu nakuja tuiendeleze Igunga.
Mimi Shishi I am currently the defacto Igunga’s MP (Power without portfolio). That Sunday Morning of the unknown date in October this year 2020, I will be declared as an official member of Parliament representing the constituency that I hold dearly in my heart and that I love the most, which is none other than Igunga.
I have fought so hard to make Igunga shine on the Tanzanian Map, now is the time to become a real lady of the people’s choice and serve them with full instruments of power’. Tukutane Mjengoni, Hapa Kazi Tu.
Shilole ni mwanamuziki anayetokea wilayani Igunga mkoani Tabora hivyo ametangaza nia ya kugombea ubunge kwenye jimbo la nyumbani kwake.