Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Shilole amefunguka na kusema kutokana na kukithiri kwa mauaji ya wapenzi hasa wanawake, anamuomba Rais Samia kusaidia itungwe sheria mpya.

Shilole ambaye kipindi kile alieleza jinsi alivyokuwa akipokea kipigo kwa aliyekuwa mumewe, Uchebe amesema;

“Tunamuomba Rais atusaidie kutunga sheria mpya kwa ajili ya kumlinda mtoto wa kike kwenye ndoa na maisha ya kawaida ili tuondoe huu ukakasi.

Kwenye ndoa kuna matukio mengi makubwa yanatokea na watu hawasemi chochote mwisho wa siku anayeathirika ni mama.

“Nipo kama mwanamke mtetezi wa wanawake wenzangu, nilikuwa namuomba Mhe Rais Samia Suluhu Hassan atusaidie kuunda sheria mpya inayomtetea mwanamke.”

Kumekuwa na matukio mengi yanayosababishwa na migogoro ya ndoa ikiwemo mauaji kutokana na kile kinachotafsiriwa kama wivu wa mapenzi hali inayotishia jamii na kuona haja ya kuwepo sheria rasmi ya kuratibu mahusiano ndani ya ndoa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *