Mwanamuziki wa Bongo fleva na muigizaji nchini, Shilole amefunguka na kuwapa neno baadhi ya vijana ambao wamekuwa wakilalamika juu ya hali ngumu ya maisha huku wengi wao wakiitupia lawama Serikali ya awamu ya tano.

Kupitia akaunti yake ya Instagram Shilole amesema amewachana baadhi ya vijana hao na kusema wamekuwa wakilalamika kuwa kuna hali ngumu ya maisha au pesa haipatikani ikiwa wao wenyewe hawahitaji kujishughulisha wamebaki kukaa vijiweni pasipo kuhangaika kutafuta mishe za hapa na pale za kuingiza kipato.

Baadhi ya mashabiki wa Shilole wamemuunga mkono kutokana na kauli yake hiyo huku wengine pia wakionyesha kutokubaliana naye wakiendelea kusema kweli maisha ya sasa ni magumu na mishe hakuna.

Shilole ameandika ‘Unalalamika hali ngumu huku umekaa’ kutokana na maneno hayo aliyoandika Shilole ameungwa mkono na baadhi ya amashabiki wake wanaomfuata kwenye matandano huo.

Maneno hayo Shilole yamekuja kufauatia baadhi ya vijana kulalamika mtaani wakidai hali ya maisha ngumu wakati wanakaa tu vijiweni.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *