Mwanamuziki wa Bongo Fleva,Shilole amefunguka na kusema kuwa Ray Kigosi ndiyo mtu aliyemsaidia mpaka akafanikiwa kisanaa.
Shilole amesema kuwa Ray Kigosi alikuwa mteja wake kwenye mgahawa aliokuwa anafanya kazi wakati huo na ndiyo wakaanza kufahamiana mpaka akamsaidia katika Sanaa.
“Kuna siku siku nilimpigia simu nikamwambia nataka kuigiza, na kuwa mimi ni mzuri kuliko Irene Uwoya, akaniambia niende ofisini kwake Sinza, nilichukua bajaji nikawakuta yupo na Johari na Uwoya waliniambia niigize namtongoza Ray” Alisema Shilole.
Ameongeza kwa kusema kuwa “Tangu nikiwa kijijini Igunga moyo wangu ulikuwa unaniambia ipo siku utakuwa maarufu, utapesa pesa, utakuwa na biashara zako, utaenda nchi za nje lakini hutafanya yote haya ukiwa hapa, ndiyo maana nikatoka Igunga kuja Dar es Salaam,”.
Pia amedai hawezi kurudiana na aliyekuwa mumewe Uchebe kwani kufanya hivyo ni sawa na kuendesha gari likiwa kwenye handbrake.