Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Shilole amewajia juu wanawake wanaotukana wanawake wenzao mitandaoni bila kujali jinisia zao na hao wanaowatukana.
Kauli ya Shilole imekuja baada ya kukumbana na matusi katika mitandao ya kijamii bila sababu yoyote jambo ambalo limetokea kumkera.
Shiloleh amefunguka na kusema kuwa amekuwa akwashangaa sana wasichana wanaokaa kutwa kutukana watu katika mitndao ya kjiamii kama hawana kazi za kufanya wakati kuna mambo mengi ya kushughulika nayo.
Shiloleh amesema kuwa aina hiyo ya wanawake wanakera na pia wanatia aibu sana wanawake wenzao , hivyo waache mara moja na kufanya vitu vingine vya maana.
Pia Shiloleh amesema kuwa watu waache kumsema vibaya msanii Chid Benz kwa sababu kwa sasa hayuko kama alivyokuwa zamani.