Aliyekuwa mbunge wa Maswa Magharibu, John Shibuda amewataka waliopokea fedha za mgao wa Escrow kuzirejesha fedha hizo.
Shibuda amesema anaona Ngeleja anatakiwa asamehewe kwa vile amefanya kitendo cha kishujaa, kukiri na kuamua kuzirejesha fedha hizo
Shibuda ametoa kauli hiyo siku chache baada ya Mbunge wa Sengerema, William Ngeleja (CCM) kurejesha Sh milioni 40.4 alizopewa na mfanyabiashara, James Rugemalira.
Pia Shibuda amesema kitendo kilichofanywa na Ngeleja ni cha kishujaa na anapaswa kusamehewa kwa kuwa ametambua kosa lake mbele ya umma.
Wakati huohuo, Shibuda amewashambulia wapinzani kwa akidai wanatakiwa kuwa na ajenda mpya kwa vile zilizopo, Rais wa sasa Dk. John Magufuli amekwisha kuzitatua kwa kiwango kikubwa.
Amesema Serikali ya awamu ya tano imo katika dunia ya mabadiliko ya mila, jadi na utamaduni na kokomesha uzembe.
Alisema ajenda ya vyama vya upinzani kama rushwa, ufisadi imenyauka na kuvitaka kutafuta sehemu ya kutokea.
Shibuda alisema serikali ya awamu ya tano inafanya vizuri huku akidai Taifa limepata Rais mwenye utumishi wachangamfu na kugusa hisia za jamii.