Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Shetta amefunguka na kusema kuwa kwasasa sio siri tena yeye na mama mtoto wake wameachana na sasa yupo kwenye mahusiano mengine.
Licha ya kuachana kwao, Shetta amesema kuwa wanashirikiana na mama watoto wake huyo kulea watoto wao wawili, Khailla na Khamla ambao wote ni watoto wa kike.
Shetta ameongeza kuwa licha ya kuwa ameachana na mama watoto wake lakini linapokuja suala la kulea watoto wapo serious sana na huwa hawataki masikhara.
Shetta aliuliza huenda labda ana mpango wa kuoa mwanamke mwingine ili amsaidie kulea watoto Shetta alisema kuwa yeye mwenyewe analea watoto wake akisaidiana na dada wa kazi hivyo anaamini yeye ni baba bora.