Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Shetta ameshauri wasanii kutokimbilia kwenye mitandao ya kijamii wanapoachana kwani huo ni ukatili wa na unyanyasaji wa kijinsia.

Shetta ameyasema hayo wakati alipokuwa akizindua shirika lake la ‘Sawa Initiative Tanzania’ linalolenga kupingana na vitendo vya ukatili wa kijinsia kwenye jamii.

Msanii huyo amesema hata yeye mwaka jana aliachana na mke wake walioishi naye miaka tisa, lakini anashukuru waliweza kuliweka sawa hilo wenyewe bila kukimbilia mitandaoni.

“Ilikuwa ni hatua ngumu sana kwangu ukifikiria ni mwanamke tumeishi naye miaka tisa na tuna watoto wawili naye, lakini sikutaka haya kuyapeleka huko mitandaoni badala yake tuliyamaliza wenyewe.

“Pia nashukuru kwa sasa tumebaki kama wazazi katika kulea watoto na tumekuwa tukitoka nao out wakati mwingine lengo ni kuwafanya watoto wetu wasijisikie vibaya na waone uwepo wa wazazi wote katika kuwalea,” amesema Shetta.

Akizungumzia kuhusu shirika lake, msanii huyo  amesema ni katika kupambana na vitendo vya ukatili wa kijinsia ambao umezidi kushamiri katika jamii.

Katika kufanya kazi hiyo, amesema wameanzisha klabu mashuleni na njia kubwa watakayoitumia katika kueneza elimu ya kupambana na vitendo hivyo ni kutumia muziki.

Katika uzinduzi huo wasanii mbalimbali walishiriki akiwemo Barnaba, Dogo Janja, Madee, Kala Jeremiah, Mwasiti, G Nako, Ommy Dimpoz na wengine wengi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *