Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Ambwene Yesaya maarufu kama AY amefunga ndoa na harusi ya pili jijini Dar es Salaam zikiwa zimepita siku kadhaa tangu afunge ndoa na mpenzi wake wa muda mrefu, Munyana Rehema ‘Remy’.

AY na Remmy walifunga ndoa Februair 10 Kigali Rwanda na harusi ikafanyika kwenye hoteli ya Golden Tulip jijini humo. Harusi ya Dar es Salaam imefanyika mwishoni mwa wiki katika hoteli ya Golden Tulip iliyopo kando ya Bahari ya Hindi, Oysterbay Jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa na wasanii mbalimbali.

Baadhi ya wasanii hao nyota wengi wao wakiwa ni wanamuziki ni pamoja na Lady Jaydee, Mwana FA, Salama Jabir, Profesa Jay (Joseph Haule), Fid Q na wengine kibao.

Sherehe hiyo imefanyika wiki tatu baada ya AY, familia yake, ndugu, jamaa na marafiki kwenda Rwanda kulipa mahali kwa ajili ya kumuoa mpenzi wake huyo wa muda mrefu.

AY amepata tuzo kibao katika muziki ndani na nje ya nchi ambapo alitwaa tuzo ya kibao bora cha Hip Hop (Usijaribu) mwaka 2017, huku akipewa tuzo ya Kisima ya video bora ya Usijaribu na tuzo nyingine kibao.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *