Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk Ali Mohamed Shein amepongeza juhudi zinazoendelea kuchukuliwa na Wizara ya Kilimo, Maliasili, Mifugo na Mazingira, ikiwa ni pamoja na azma ya kuupandisha hadhi msitu wa Masingini kuwa msitu wa hifadhi.

Dk Shein amesema Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) itaendelea kuziimarisha sekta za kilimo, mifugo na uvuvi kwa kutambua umuhimu wake mkubwa kwa maendeleo ya nchi pamoja na wananchi wake.

Alisisitiza haja ya kuendeleza mchakato wa kuanzisha kiwanda cha matrekta hapa nchini kama ilivyoamua serikali, kwani tayari hatua za awali zimeshafanyika kwa kuzingatia kuwa kilimo huimarika panapokuwa na huduma za matrekta.

Alieleza kuwa, haja kwa uongozi wa wizara hiyo kuendelea na juhudi za kuulinda msitu huo ili kuepuka kuja kuvamiwa kwa ujenzi huku akitumia fursa hiyo kuitaka wizara hiyo kusimamia na kudhibiti vyema maliasili zisizorejesheka ili kuepuka athari zaidi za hapo baadaye.

Mapema Waziri wa Kilimo, Malisili, Mifugo na Uvuvi, Hamad Rashid Mohamed alisema kuwa sekta ya kilimo inajumuisha sekta ndogo za mazao, mifugo, uvuvi na misitu bado inaendelea kuwa ni mhimili mkuu wa uchumi wa Zanzibar na inatoa mchango wa moja kwa moja katika kujikimu kimaisha.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *