Staa wa muziki wa dance hall kutoka nchini Ghana, Shatta Wale amejikuta mikononi mwa polisi baada ya kuongopa kuwa amepigwa risasi na mtu asiyejulikana.


Shatta Wale alitoa taarifa hiyo kupitia kwenye mitandao ya kijamii jambo ambalo lilizua taharuki kwa uma. Serikali ya nchini Ghana imethibitisha kumkamata Shatta Wale kwa uchunguzi Zaidi.


Mnamo October 18,2021 Shatta Wale alitumia mitandao ya kijamii kuchapisha taarifa kuwa amepigwa risasi na mtu asiyejulika.

Na ilipofika October 19,2021 aliomba radhi kwa kutoa taarifa za uongo kwenye mitandao ya kijamii nchini humo na kusamehewa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *