Muigizaji wa Bongo Movie, Shamsa Ford amewaponda wakongwe wenzake wa tasnia ya filamu kuwa hawana jipya hivyo kutaka sura mpya kujitokeza kwenye fani hiyo.
Shamsa amesema hayo baada ya kuona wasanii wakongwe wa Bongo Movie kuwa kimya kwa muda mrefu.
Shamsa alifunguka ishu hiyo wiki iliyopita alipokuwa akifanya usahili wa wasanii chipukizi watakaouza nyago kwenye sinema mpya iitwayo Saa Imetimia.
Shamsa aliwataja mastaa wakubwa kama Aunt Ezekiel, Irene Uwoya, Jacqueline Wolper na wengineo kuwa wanashindwa kuonesha jipya kwenye tasnia hiyo na kuwafanya mashabiki kuhamia kwenye sinema za nje.
Tasnia ya filamu Bongo kwasasa imeshuka kutokana na waigizaji wake kukaa kimya bila kuingiza kazi sokoni kama ilivyokuwa hapo awali.