Muigizaji wa Bongo Movie, Shamsa Ford amefunguka na kuwataka watu waache roho ya ubinafsi nay a kikatili kwa binadamu mwingine.

Kupitia ukurasa wa Instagram wa Muigizaji huo wa Filamu ameandika…

“Nakusihi ndugu yangu usiwe na roho ya ubinafsi,roho ya kikatili,roho mbaya,ubinafsi,roho ya visasi siku zote kumbuka maisha yetu ya Duniani ni ya kupita.usijione ww ni bora kuliko mwingine kwasababu umewazidi wenzio uwezo,usimdharau au kumnyanyasa masikini kila kitu unachokiona Duniani au ulichonacho utakiacha.

Waliokufa jana walikuwa na mipango mingi siku ya leo lakini Mwenyezi Mungu amewaachukua.Inshaallah Mwenyezi Mungu atupe mwisho mwema .
Alhamdulilah Mwenyezi Mungu amenipa nafasi nyingine ya kuiona siku ya leo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *