Muigizaji wa Bongo Movie, Shamsa Ford amewapa somo mashabiki wake akiwaambia wasiwe wajuaji sana hata kama wana majibu wanyamaze kwa sababu wanaweza kujibu kitu, halafu wakatafsiriwa vibaya.
Amesema; “Maisha yanahitaji unyenyekevu wa hali ya juu, ukitaka kufanikiwa katika maisha basi jitahidi sana kuwa mnyenyekevu kwa kila mtu hata yule unayemuona hafai ipo siku atakufaa.
“Muda mwingine ni bora uonekane mjinga, huna akili lakini ya kwako yanaenda. Usiwe mjuaji sana kila siku baki kuwa mwanafunzi utafaidika.
“Pia jitahidi kukaa kimiya hata kama una jibu maana unaweza ukajibu jambo kwa nia njema likaonekana baya.”