Muigizaji wa Bongo Movie, Shamsa Ford amewajia juu mashabiki wanaomponda kwa kitendo cha yeye kuuza duka mwenyewe badala ya kumuweka mtu amuuzie.
Mwanamuziki huyo amesema hayo baada ya baadhi ya watu kumshambulia kuwa kwa umaarufu wake atakiwi kuuza duka anatakiwa atafute kijana wa kuuza duka hilo.
Shamsa ambaye anamiliki duka la nguo na mumewe Chid Mapenzi lililopo Kinondoni jijini Dar es Salaam ameema haoni aibu yoyote kuuza mwenyewe dukani hapo kwa sababu ustaa bila kipato chochote ni sawa na mzigo tu hivyo wanaomponda kwenye mitandao ya kijamii wanajisumbua.
“Unajua kuna watu nawashangaa sana wananiambia si nitafute mtu akae dukani halafu mimi nifanye nini? Mastaa wengi wamezoea kulala tu sasa mimi siwezi unapopata fursa ni lazima uitumie ipasavyo,”.
Muigizaji huyo ameanza kuuza duka baada ya kuolewa na mfanyabiashara wa maduka ya nguo nchini maarufu kama Chid Mapenzi.