Waziri Mkuiu, Kassim Majaliwa amesema kuwa Serikali  imepeleka Sh1.92bilioni  katika Halmashauri ya mji wa Nanyamba wilayani Mtwara kwa ajili ya ujenzi na uboreshaji wa vituo vya afya.

Waziri Mkuu ameeleza hayo wakati akizungumza na wakazi wa halmashauri hiyo, akiwa katika ziara mkoani Mtwara.

Amesema fedha hizo zilitolewa na Serikali ili kuimarisha upatikanaji wa huduma za afya kwa wananchi, kwamba Sh1.2bilioni zimetolewa kwa ajili ya ujenzi wa kituo cha afya Kata ya Njengwa, ambapo aliwasisitiza watendaji kutobadilisha matumizi.

Amebainisha kuwa ujenzi huo utahusisha chumba cha upasuaji, maabara, chumba cha kujifungulia, jengo la mama na mtoto na wodi ya wanawake na wanaume, eneo la kuchomea taka na chumba cha kuhifhadhia maiti.

AMajaliwa amewataka wananchi hao kuendelea kuiunga mkono Serikali ambayo imedhamiria kuwatumikia ili waweze kupata maendeleo.

Amesema Serikali inatarajia kuipitia upya sheria ya elimu pamoja na sheria ya mtoto ili kuweka masharti ya kumlinda mtoto wa kike hususani kudhibiti mimba kwa wanafunzi.

Awali, Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Gelasius Byakanwa amesema Serikali itawachukulia hatua watu wote watakaobainika kuwapa watoto wa kike dawa za uzazi wa mpango ili kuwazuia wasipate mimba.

Amesema wanafunzi wa kike katika halmashauri hiyo wamebainika kuwa wanatumia dawa za kuzuia mimba wakiwa shuleni, hivyo kuwaruhusu kushiriki katika matendo yasiyokuwa ya kimasomo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *