Serikali ya Jahmhuri ya Kidemokrasia ya Congo imekataa kuhudhuria mkutano wa kuchangisha fedha za msaada kwa janga linaloshuhudiwa nchini ikisema Umoja wa mataifa umetilia chumvi ukubwa wa tatizo lililopo.
Katika mkutano maalum mjini Geneva Uswizi, Umoja wa Mataifa ulikuwa unatarajia kuchangisha fedha za kukabiliana na janga la kibinaadamu nchini Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo.
Mashirika ya misaada yanasema zaidi ya watu milioni 5 wamelazimika kuyatoroka makazi yao kwasababu ya mapigano katika sehemu tofauti za nchi hiyo kubwa.
Lakini serikali ya DRC imekataa kuhudhuria mkutano huo wa ufadhili ikisema kwamba hali inafanywa kuwa mbaya wakati ni kinyume.
umedhamiria kuchangisha dola bilioni 1.7 kupunguza uzito wa inachotajwa na Umoja wamataifa kuwa ni janga kubwa la kibinaadamu nchini Congo.
Mpaka sasa serikali ya DRC haijajibu mwaliko wa Umoja wa mataifa ikisema taasisi hiyo kuu imetilia chumvi hali halisi nchini na ukubwa wa tatizo lililopo.
Mashirika ya misaada yanasema watu milioni tano wamelazimika kuyatoroka makazi yao kutokana na ghasia, mapigano, njaa na ukosefu wa utulivu na kwamba maelfu ya raia wa Congo wamelazimika kutafuta hifadhi magharibi mwa Uganda.
Wanaharakati wa kutetea haki za binaadamu ndani ya DRC wamekumbwa wasiwasi kutokana na hatua hiyo ya serikali kususia mkutano huo mkuu mjini Geneva.