Waziri Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk Harrison Mwakyembe amemtembelea msanii nguli wa filamu, Amri Athuman maarufu mzee Majuto na kueleza kuwa Serikali inabeba jukumu la matibabu yake.

Mzee Majuto alilazwa Aprili 23 baada ya kuzidiwa ghafla kutokana na kidonda cha operesheni ya henia aliyofanyiwa Julai mwaka jana jijini Tanga.

Akizungumza katika tukio hilo Dk Mwakyembe amesema Serikali imeamua kumpeleka mzee Majuto nchini India kwa ajili ya matibabu zaidi.

Amesema matibabu atakayopata mzee Majuto akiwa Muhimbili na akiwa nchini India yatagharamiwa na Serikali.

Katika hatua nyingine, kampuni zilizowahi kufanya kazi na mzee Majuto zimeitikia wito wa kumchangia huku Dk Mwakyembe akitoa wito kwa wadau mbalimbali kuendelea kumchangia ili kuwezesha familia yake kujikimu katika kipindi hiki ambacho anapatiwa matibabu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *