Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu amesema kuwa serikali imeanza kulipa deni wanalodaiwa na Hospitali ya Apollo nchini India.

 Hayo ameyasema leo wakati alipokuwa akizindua bodi ya Wadhamini wa Taasisi ya Tiba ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI).

Waziri Ummy amesema kuwa Hospitali ya Apollo inaidai Tanzania kiasi cha shilingi bilioni 30 na kwamba wameshaanza kulipa deni hilo.

Tulikuwa tunapeleka wagonjwa wengi kufuata matibabu nje ya nchi, tumeanza kulipa deni hilo na tunashukuru idadi imepungua hadi wagonjwa 304 mwaka 2016 kutoka wagonjwa 533 2015 sawa na asilimia 45.

Kutokana na deni hilo huenda Hospitali hiyo ikasitisha kupokea wagonjwa kutoka nchini Tanzania kutokana na deni kubwa inayodai.

Hospitali ya Apollo nchini India imekuwa ikipokea wagonjwa wanaosumbuliwa magonjwa ya moyo kutoka Tanzania ambapo walikuwa wakitibiwa kwa mazungumzo maalumu kati ya Serikali na Hospitali hiyo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *