Mchezaji tenisi namba moja kwa ubora kwa upande wa wanawake, Serena Williams ametolewa  kwenye mashindano ya wazi maarufu kama US Open yanayofanyika jijini New York nchini Marekani baada ya kufungwa na Karolina Pliskova kutoka Czech kwenye hatua ya nusu fainali.

Willams amefungwa jumala ya seti 6-2 7-6 (7-5) kwenye hatua hiyo ya nusu fainali kwenye mashindano hayo ya US Open yanayondelea nchini Marekani.

Mchezaji huyo alikuwa anataka kuweka rekodi kwa kushinda tuzo ya grand slam mara ya 23 lakini ameshindwa kufanya hivyo kutokana na kutolewa kwenye hatua ya nusu fainali.

Lakini kwa sasa anabakia kushikilia rekodi na mchezaji wa zamani Steffi Graf baada ya kushinda mataji 22.

Matokeo hayo yana maana kwamba Serena Williams sasa atapitwa kwenye orodha ya wachezaji bora na Mjerumani Angelique Kerber.

Karolina Pliskova: Mchezaji tenis aliyemtoa Serena Williams kwenye mashindano ya US Open.
Karolina Pliskova: Mchezaji tenis aliyemtoa Serena Williams kwenye mashindano ya US Open.

Mjerumani huyo alimfunga raia wa Denmark Carolina Wozniacki 6-4 6-3 kwenye mashindano hayo.

Karolina Pliskova anatarajia kukutana na Angelique Kerber kwenye fainali ya mashindano hayo ya US Open yanayoendelea jijini New York nchini Marekani.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *