Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Ben Pol amesema kuwa katika hifadhi zote nchini, anapendelea zaidi kutembelea hifadhi ya Taifa ya Serengeti kwa kuwa ina eneo kubwa na mandhari tofauti.
Ben Pol amesema kwamba katika nafasi yake ya ubalozi aliyoteuliwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Selemani Jafo, ni ya kusimamia udhibiti wa taka ngumu.
“Kivutio changu pendwa cha utalii ni Serengeti sababu ina scenaries tofauti tofauti nyingi, unaweza ukawa Serengeti ukajiona upo Manyara, mandhari tofauti na ina idadi kubwa sana ya wanyama ikilinganishwa na mbuga zingine.
Msanii huyo wa Bongo Fleva amesema kuwa kwasasa hivi anapendelea sana kwenda Serengeti hivyo kwake ni kivutio Zaidi.