Mshauri wa haki za picha na matangazo za msahmbuliaji wa Atletico Madrid, Antoine Griezmann amemtaka mshambuliaji kuipokea ofa ya Man United na kusaini kuichezea klabu hiyo.

Mshauri huyo, Sebastien Bellencontre amedai kuw auhamisho huo unaotarajiwa kuwa mkubwa zaidi duniani utafanya pande zote zinazohusika kupata faida maradufu.

Griezmann aliyewahi kukaririwa akidai David Beckham amekuwa mchezaji wake kipenzi na ndio maana anavaa namba 7 na jezi ya mikono mirefu anatarajia kukabidhiwa jezi namba 7 endapo atajiunga na United.

Mshauri wake wa biashara, Sebastien Bellencontre anaamini kukamilika kwa dili hilo kutakuwa na faida kimichezo na kibiashara kwa pande husika.

‘Ninaposoma makala kuhusu uhamisho huo wa kwenda Manchester United , ninahamasika sana na ninaamini itakuwa fursa nzuri sana kibiashara’. Bellencontre ameliambia jarida la So Foot. 

‘Atachezea timu ya zamani ya Beckham, ambaye ni kipenzi chake na akiwa na namba ya mkongwe huyo mgongoni. Itakuwa fursa adhimu sana sokoni’.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *