Mshambuliaji wa Arsenal, Alexis Sanchez ameisadia klabu yake kutoka nyuma na kupata ushindi wa mabao 3-1 dhidi FC Cologne katika mechi ya Europa ligi iliochefanyika jana katika uwanja wa Emirates.
Mechi hiyo hatahivyo haikuanza katika muda iliopangiwa baada ya maelfu ya mashabiki wa Cologne kuwasili katika uwanja wa Emirates bila tiketi na baadaye kuzozana na wanaowakaribisha wageni ndani ya uwanja huo.
Na mechi ilipoanza , Cologne ilichukua uongozi baada ya Jhon Cordoba kumfunga kipa David Ospina akiwa maguu 40.
Mshambuliaji Olivier Giroud alipiga nje kichwa cha wazi akiwa maguu sita pekee karibu na goli
Lakini mchezaji wa ziada Sead Kolasinac alisawazisha kabla ya Sanchez kufunga bao la pili kwenye mechi hiyo.
Beki wa kulia wa Arsenal Hector Bellelin baadaye alifunga bao la tatu huku kiungo wa kati wa Arsenal Jack Wilshere akiichezea klabu hiyo kwa mara ya kwanza tangu Agosti 2016.