Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amesema kuwa hivi sasa kuna changamoto ndogo za upungufu wa dawa nchini.

Mheshimiwa Samia ametoa kauli hiyo leo Jijini Dar es salaam wakati akiweka jiwe la msingi la ujenzi wa jengo la wazazi katika Hospital ya Mwananyamala, jengo linalojengwa kwa ufadhili wa Amsons Group of Companies.

 

Makamo wa Rais ametoa kauli hiyo ikiwa imepita siku moja tu tangu Waziri wa Afya Mheshimiwa Ummy Mwalimu alipotangaza kuwa hakuna uhaba wa dawa nchini.

Amesema kuwa hiyo ni changamoto ya muda mfupi ambayo tayari serikali imechukua hatua za haraka kuhakikisha kuwa hakutatokea upungufu wa dawa tena.

 

Amemuagiza mkuu wa mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda kwa muda wa miezi mitatu kutafuta magari mawili ya kubeba wagonjwa katika Hospital ya Mwananyamala na Hospital hiyo iweke mpango mkakati mzuri wa matumizi ya fedha zake inazopata ili kusaidia serikali kutatua changamoto zake.

 

Kwa upande wake Mganga Mfadhi wa wa Hospitali ya Mwananyamala Dkt. Daniel Nkungu ameiomba serikali kulipa madeni ya watumishi wanaoidai serikali kwa kipindi cha miaka mitatu pamoja na kumaliza changamoto ya ukosefu wa vifaa tiba.

 

Naye Waziri wa Utumishi Angela Kairuki ameahidi kufanyia kazi tatizo la malipo ya watumishi na uhaba wa watumishi katika hospitali hiyo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *