Mshambuliaji wa Genk, Mbwana Samatta na nahodha wa Taifa Stars atakaa nje kwa wiki sita akiuguza majeraha ya goti.
Samatta aliumia goti wiki iliyopita wakati akiichezea Genk dhidi ya Lokeren na kulazimika kutolewa nje katika dakika ya 40.
Samatta ameonekana kupata maumivu katika goti lake katika misuli na mifupa miepesi ambayo kitaalamu inajulikana kama Meniscus.
Kuumia kwa Samatta ni pengo kwa Genk lakini pengo pia katika kikosi cha Taifa Stars ambayo yeye ni nahodha.