Meneja wa mwanamuziki wa Bongo Fleva, Diamond Platnumz, Salaam SK amewajibu baadhi ya watu wanaomsema vibaya mwanamuziki huyo baada ya kutoka kwa wimbo wake ‘GIDI’.
Kwa upande wa Mwanamuziki wa HipHop Tanzania, Wakazi ameamua kuuhamishia Mjadala huo kwenye Mtandao wa Instagram na kundika Maoni yake juu ya ishu hiyo..
Ameandika WAKAZI..!! DIAMOND UKIWEZA FUTA HIYO SCENE!
Nilivyosikia wimbo wa Diamond “Gidi” nikajua ameuita hivyo sababu sababu ya Wanaija and honestly it feels like something Burnaboy would do. Ila nilivyoona Video, na kuona Cowboy theme, nikasema au ndio maana ni Gidi as in “Giddy Up”… All in all, nikasema labda ni double entendres, na kiukweli color palettes za vidoe ni konyo sana!
Ila nimekuja kushtuka kuona ile CONFEDERATE FLAG hapo huu. Hiyo bendera kwa marekani ina historia ya kibaguzi, na mtu yeyote anayeitumia lazima atawachefua Black Americans. Sijui ni nani ali suggest iwekwe, ila kiukweli haikuwa idea nzuri. Najua tunataka ku-breakthrough kimataifa, ila ni muhimu kuwa tunajaribu kujifunza culture za watu, na kuelewa vizuri hasa pale ambapo tunaanza kuazima vitu vyao kwenye kazi zetu tusijeingia CHA KIKE!
Pia ameandika Diamond pasipo kudhamiria au kujua, anaweza jikuta connection yake yote ya Marekani akaipoteza kwa kitu kidogo tu kama hicho kibendera! If possible anaweza edit the video, au kuombea wasione na wasizingatie, maana frankly speaking market kubwa bado ni huku kwetu ambako hatujui wala hatujali.
Sallam SK kupitia Ukurasa wake wa Twittwer ” ameandika Mkiwa na jambo lenu mnanipigia private, mkitaka kukosoa biashara yangu mnaandika mitandaoni.