Mwanamuziki wa nyimbo za asili, Saida Karoli amesema kuwa amefurahi sana kupata nafasi ya kutumbuiza kwenye tamasha la Sauti za Busara kwa mara nyingine.

Saida Karoli ameahidi kufanya vyema katika tamasha hilo litakalofanyika visiwani Zanzibar mwaka huu.

Mwanamuziki huyo amesema kuwa kweke imekuwa bahai kupata nafasi ya kwenda kutumbuiza kwenye tamasha hilo kwani mara ya mwisho ilikuwa mwaka 2005 wakati akifanya vizuri kwenye muziki wake.

Pia amesema kuwa Sauti za Busara ni sehemu nzuri ya kukutana na kubadilishana mawazo na  fikra na baadhi ya wasanii wanaokutana kwenye tamasha hilo.

Tamasha la Sauti za Busara ufanyika kila mwaka mwezi wa pili visiwani Zanzibar na hukutanisha wasanii tofauti tofauti katika muziki kutoka nchi mbali mbali.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *