Mwanamuziki mkongwe wa muziki wa asili, Saida Karoli amefunguka na kusema kwamba ukosefu wa pesa na mapromota waongo ndicho kitu pekee kilichomfanya apotee katika ramani ya muziki nchini.
Saida amefunguka hayo baada ya ujio wake mpya kwa kuachia video inayokwenda kwa jina la ‘Orugambo’.
Mwanamuziki huyo ameongeza kwa kusema kwamba aliamua kurudi kijijini kwao baada ya kukosa muelekeo maalumu wa maisha yake baada ya kufeli kwenye muziki.
Saida Karoli amsema kuwa asingeweza kufanya kitu chochote bila kuwa na pesa, mapromota walimuangusha sana kipindi cha nyuma kitu ambacho kilinifanya nipotee.
Kuhusiana na suala la kutengeneza muziki mzuri, Saida amesema muziki wake unaonekana kuwa mzuri kwa sababu anatumia vitu vya asili katika kuutengeza .
Saida amewahi ametamba na nyimbo mbalimbali ikiwemo, Maria Salome, Kizunguzungu na nyinginezo nyingi zilibamba mashabiki enzi za nyuma.
Mwanamuziki huyo kwasasa anatamba na wimbo wake unaokwenda kwa jina la ‘Orugambo’ ambapo wiki iliyopita alifanya uzinduzi wa video hiyo.