Aliyekuwa mpenzi wa mwanamuziki wa Bongo Fleva, Diamond Platnumz, Zary The Boss Lady ametua Tanzania kwa zoezi la kurejesha kwa jamii kuelekea siku ya hedhi salama duniani Mei 28 mwaka huu.

Zari yuko Tanzania ambapo katika sehemu ya zoezi hilo mapema Mei 14 2022 ametoa taulo za kike kwa shule za msingi na sekondari kwa wanafunzi wa kike kuelekea siku hiyo inayoadhimishwa kila mwaka duniani.

Zari kama balozi wa Dowecare akishirikiana na kampuni hiyo wametoa msaada huo wa taulo za kike kwa shule za Msingi na Sekondari za wilaya ya Misungwi.

Zari amesema kuwa yeye ameachana na Diamond lakini hakuachana na Tanzania hivyo atakuwa anakuja nchini kila inapohitajika kufanya hivyo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *