Klabu ya Yanga imefunga sababu ya kupeleka timu  B vijana chini miaka 20 kuchuana na Kombaini ya majeshi kwenye sherehe za Muungano zilizofanyika jana mkoani Dodoma.

Katika taarifa iliyotolewa na Makamu Mwenyekiti wa Yanga SC, Clement Sanga amesema kulikuwa na dosari kadhaa katika kufikia makubaliano ya ushiriki wa mechi hiyo ya kirafiki.

Pia Sanga amesema kuwa sababu nyingine ni ukaribu wa ratiba za michuano ya nusu fainali za FA dhidi ya Mbao Fc mwishoni mwa wiki.

Pamoja na hayo, Sanga amewaomba radhi mashabiki wote waliosikitishwa na uamuzi huo kwa namna moja ama nyingine huku akiwasii waendelee kuungana na kushikamana ili waweze kutwaa makombe wanayoshiriki kwa sasa.

Kwa upande mwingine, timu ya Yanga U20 iliweza kutoka sare ya bao 1-1 ambapo goli hilo la Yanga lilifungwa na Yusuph Mhilu kwenye dakika 52 ya mchezo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *