Muigizaji wa Bongo Movie, Wema Sepetu amefunguka sababu ya kufanya movie na wasanii wa Ghana na kuwatosa wasanii wa Bongo.

Wema ambaye wiki iliyopita alizindua movie yake mpya D.A.D Mlimani City jijini Dar es Salaam ambayo amefanya na msanii mkubwa kutoka nchini Ghana Van Vicker.

Muigizaji huyo amesema kuwa aliamua kwenda kufanya movie hiyo nchini Ghana ili kubadilisha mazingira ya uigizaji ili aweze kuteka soko la filamu la nchini Ghana kutokana na movie ambaye imefanywa na wasanii wengi wa Ghana.

Wema amesema kuwa yeye ndiyo aliyemtafuta Van Vicker ili afanye nae kazi lakini pia alimwambia atafute waigizaji wengine wa nchini Ghana.

Pia muigizaji huyo ambaye ni miss Tanzania mwaka 2006 amesema kuwa mazingira ya Ghana ni mazuri sana kwani wana kila kitu wanachohitaji katika uigizaji wanapewa na serikali yao mfano wakitaka kuigiza hata Mahakamani wanapewa ruhusa ya kufanyia hivyo.

Wema ameongeza kwa kusema kuwa hata kama wakihitaji benki au hata uwanja wa ndege serikali yao inawasaidia tofauti na Tanzania mfano ukihitaji kuigiza katika uwanja wa ndege wanakwambia ufanyie nje na sio ndani.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *