Mwanamuziki mkongwe wa Bongo Fleva, Soggy Doggy amefunguka sababu zilizomfanya ajiweke pembeni kwenye ramani ya muziki wa hip hop kwa muda mrefu.

Soggy Doggy amesema ushindani uliopo kwenye soko la muziki na gharama za ufanyaji wa video zimekuwa ni kubwa, kitu ambacho ni kigumu kukimudu hasa kwa mtu mwenye majukumu kama yeye.

Mwanamuziki huyo amezungumza  hayo na kusema muziki unahitaji matumizi makubwa ya pesa kitu ambacho kilimfanya arudie kazi yake ya utangazaji lakini hata kama akitaka kurudi kwenye ‘game’ lazima arudi kama vijana wa sasa ili muziki wake uonekane bora.

Pia Soggy amewashauri vijana wa sasa wanaofanya muziki kutumia muda mrefu kwenye kuandika na kuhariri mashairi yao ili kuepuka adha za kufungiwa kazi zao na vyombo husika.

Mwanamuziki huyo kwasasa amejikita kwenye utangazaji katika kituo cha Radio cha EFM kilichopo Dar es Salaam.

 

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *