Mwananmuziki wa Bongo Fleva, Rayvanny amefunguka sababu ya kuficha uhusiano wake mpya baada ya kuachana na mpenzi wake Feyvanny.
Rayvanny amesema kuwa, kuweka uhusiano hadharani ni uamuzi wa mtu mwenyewe hivyo hawezi kusumbuliwa na watu kuhusu mahusiano yake mapya.
“Hakuna binadamu ambaye anakosa uhusiano, lakini kuweka hadharani au kutokuweka ni uamuzi wa mtu.
Pia amesema kuwa Ninachojua mpenzi ni wako sasa unavyoweka mtandaoni watu wanaona kila kitu, wapo ambao wataanza kurusha mishale yao, hapo unabaki kujiuliza mpenzi wako atakwepa mishale yote’’
Rayvanny ameachana na mzazi mwenzake, mwanamitindo na mjasiriamali, Fahyvanny aliyezaa naye mtoto mmoja wa kiume aitwaye Jaydanny.