Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Jeshi la Polisi Mkoani Morogoro, Kamanda Ulrich Matei amethibitisha kukamatwa Nay wa Mitego usiku wa kuamkia leo mkoani Morogoro.
Kama Ulrich Matei ametoa sababu kubwa ya kukamatwa kwa msanii huyo ni kutokana na kutoa wimbo unaofahamika kwa jina la ‘Wapo’ ambao anadai unaikashfu Serikali iliyopo maradakani.
Kamanda Matei amesema shauri la Nay wa Mitego lipo jijini Dar es Salaam hivyo msanii huyo atasafirishwa na kupelekwa Dar es Salaam kuhojiwa kwa Mkuu wa Upelelezi wa mkoa.
Habari za kukamatwa kwa Nay wa Mitego zimeanza kusambaa leo baada ya yeyey mwenyewe kuthibitisha kukamatwa kwake baada ya kupost ujumbe kupitia ukurasa wake wa Instgram.
Kupitia akaunti yake Instagram Nay ameandika “Nimekamatwa kweli. Muda Huu nikiwa hotel Morogoro baada ya kumaliza Kazi yangu iliyo ni leta. Napelekwa Mvomelo Police. Nawapenda Watanzania wote.”